Friday, October 26, 2012

HAKUNA LISILOWEZEKANA.

                          



Hakika Mungu si mchoyo na hivyo hawezi kukunyima kila kitu.Wakati wanaharakati wa haki za binadamu kila pande Duniani wakiendelea kulalamikia miundombinu isiyo rafiki kwa walemavu,mlemavu huyu alionekana akiendesha baiskeli ya miguu miwili kando kando ya Barabara ya Msasani, jijini Dar es Salaam,hivi karibuni.
Hii inatafsiriwa kama ujumbe kwa walemavu wote kwamba hakuna lisilowezekana endapo watathubutu kwani kwa hali ya kawaida ni kama ndoto au jambo lisilowezekana kumuona mlemavu kama huyu akiendesha baiskeli yenye magurudumu mawili.Hii ni kutokana na ukweli bayana kwamba wengi wetu tumezoea kuwaona walemavu wakiendesha baiskeli zenye miguu mitatu ama minne.

No comments:

Post a Comment