Friday, October 26, 2012

TAKRIBANI WAFANYAKAZI 78 MGODI WA RESOLUTE (T) LIMITED NZEGA WAPUNGUZWA KAZI.

                                  Katika kile kinachosemekana kuwa ni hatua za mwanzo za kufungwa kwa mgodi wa dhahabu wa Lusu uliopo katika kata ya Lusu wilayani Nzega mkoani Tabora unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Resolute Goldmine (T) Limited,wafanyakazi takribani 78 wamepunguzwa kazi mwishoni mwa mwezi September.
Wakizungumzia sakata hilo,baadhi ya wafanyakazi hao wamesema zoezi hilo litakuwa endelevu na litafanyika kila mwisho wa mwezi ama wakati wowote endapo kampuni itaona inafaa kufanya hivyo.Aidha wafanyakazi hao wamesema kuwa Kampuni imechukua maamuzi hayo kutokana na kupungua kwa shughuli za uzalishaji katika kampuni hiyo."Shughuli za uzalishaji zimepungua sana kwa sasa,tena kuna mpango wa kupunguza wafanyakazi wengine tarehe 15 mwezi huu na sio mwisho wa mwezi tena".Alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo aliyebahatika kuukwepa mchujo wa kwanza.
Aidha taarifa za ndani kutoka katika mgodi huo zinadokeza kuwa mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu kampuni ya Casspian ambayo inafanya shughuli za uchimbaji katika mgodi huo haitakuwa na chake tena.
"Mali haijaisha,tena bado ipo nyingi sana ila nahisi mkataba ndo umekwisha au kuna issue nyingine inaendelea na kuna uwezekano kampuni nyingine ikaja kutake over".Alisema pia mmoja wa wafanyakazi aliyenusurika katika mchujo huo wa kwanza.


Itaendelea..............

No comments:

Post a Comment